MKATE WA MAYAI NA ZABIBU
Vipimo
· Mayai 4
· Sukari ¼ Kikombe
· Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula
· Hiliki ya kusaga ½ kijiko cha chai
· Baking powder ½ Kijiko cha chai
· Zabibu kavu ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, hiliki na vunja juu yake mayai yote manne.
Changanya sukari, hiliki na mayai kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.
Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto.
Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge.
Mimina unga ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.
Tupia zabibu juu ya mchanganyiko wako.
Ingiza sufuria ndani ya jiko (oven) kwa dakika 20 kisha utoe.
Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
Trik Menang Bermain Situs Judi Sabung Ayam Online Yang Jarang Diketahui Klik Di Sini
JibuFutaInformasi Terlengkap Mengenai Sabung Ayam
https://sateayambv.blogspot.com/2018/12/judi-sabung-yaitu-kekhasan-masyarakat.html/