Vinavyohitajika
Unga wa ngano magi 3
Maziwa ya maji magi 1
Hamira vijiko 2 vya kulia
Maji kiasi
Chumvi kijiko 1 cha kulia
Mafuta ya kupikia au siagi vijiko 2 vya kulia
Namna ya kutayarisha
Changanya unga, hamira, chumvi pamoja na maziwa vichanganye pamoja.
Ongezea maji kidogo kidogo mpaka uchanganyike na uuanze kuukanda.
Ukande vizuri mpaka ukandike ulainike.
Chukua tray zako upake mafuta na ukate madonge ya unga upange kwenye tray uwache uumke na uchome kwenye oven gas mar 7 au Jiko la umeme 200.
Kidokezo
Hakikisha madonge ya unga yasiwe makubwa kama ya mikate ya kusukuma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni