Vinavyohitajika
1. Nyama ya kusaga ¼ kilo
2. Mayai 4 makubwa
3. Papi za sambusa 3
4. Chumvi
5. Pilipili mtama (manga) ½ kijiko cha kula
6. Pilipili boga ¼
7. Kotmiri ½ ya kisahani cha chai
8. Thomu na tangawizi kijiko 1 cha chai
9. Ndimu kijiko 1 cha chai
10. Unga wa toast (bread crumble)
11. Mafuta ya kupikia
Namna ya kutayarisha
· Katakata pilipili boga vipande vidogo vidogo.
· Chambua majani ya kotmiri .
· Kausha nyama yako kwa kutia thomu na tangawizi, pilipili manga,chumvi pamoja na ndimu.
· Iwache ipoe.
· Piga mayai yako 3 kama kiwanda uyamimine kwenye chuma cha mafuta ya moto (weka kijiko kimoja na nusu cha chakulia).
· Tandaza nyama yako ndani kiwanda na utie pilipili boga juu yake na ikifuatiwa na kotmiri.
· Kigeuze kiwanda chako upande wa pili na uhakikishe kimewiva vizuri.
· Ukisha maliza kupika kiwanda.
· Weka kaki zako kwa mpangilio ufuatao:-
1. Weka papi yako ya kwanza na uipake ute wa yai pembezoni.
2. Na weka papi yako ya pili juu yake zishikane.
3. Paka tena ute wa yai mwisho wa papi zako mbili
4. Weka kaki yako ya tatu mwisho wa kaki yako ya pili ili zishikane upate urefu unaohitajika
· Kiweke kiwanda chako juu ya kaki zako mbili ulizounganisha mwanzo.
· Anza kuroll mpaka mwisho na hakikisha unapata mviringo uliokaa sawa.
· Tayari kwa kukata slice za mviringo huo.
· Paka mviringo wako yai pembeni.
· Ugaragize kwenye unga wa toast.
· Anza kuzichoma egg rolls zako kwa moto mdogo mdogo kwenye chuma cha kuchomea lakini usiweke mafuta mengi ( weka vijiko vya chakula 4 vya mafuta kwa kila egg roll 8).
· Vitowe na tayari kwa kuliwa
Kidokezo
Ni vizuri kuhimiza kuvikata wakati yai likiwa limoto na kaki kabla ya kukauka kwani ukichelewa utapata tab
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni