Vinavyohitajika
Nazi kipande 1
Nnga magi 4
Chumvi
Sukari kijiko 1 ½ cha chakula
Ute wa yai 1
Hamira vijiko 3 vya chakula
Ufuta wa kutosha
Namna ya kutayarisha na kupika
· iroweke nazi yako kwenye blender kwa maji ya vuguvugu na uisage vizuri
· weka unga wako ndani ya bakuli na utie hamira, chumvi ,sukari na ute wa yai
· changanya unga wako kwa nazi uliyokwisha isaga (tui)
· upige unga wako (tofauti na kuukanda) namaanisha unga huu unazidi maji
· ukisha changanyika vizuri unga wako ufunike na usubiri uumke
· ukisha umka
· weka bakuli la maji na utie chumvi kiasi(lakini ukiyaonja chumvi ijitokeze)
· weka chuma chako kwenye jiko kipate moto rushia maji yenye chumvi kwenye chuma cha moto
· teka unga wako kwa kiganja cha mkono una uutandaze kwenye chuma
· nyunyiza ufuta juu ya mkate wako kabla haujakauka
· utie kwenye grill hapo utaumuka na kuwiva kuwa rangi nzuri ya kuvutia
· rejesha tena juu ya jiko kwa moto wa kiasi na uupake mafuta kwa brash
· utoe na uuweke sahanini tayari kwa kuliwa.
Kidokezo
Ukitia yai na kiini chake cha manjano utachelewa kuumka na hautakuwa na rangi nzuri ya kuvutia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni