Alhamisi, 16 Oktoba 2014

Keki ya kawaida

Keki ya Kawaida
 
Vinavyohitajika

·         Siagi ya baking 500g – nusu kilo.
·         Sukari 500g – nusu kilo.
·         Unga  wa ngano 1000g – kilo moja.
·         Arki rose kijiko 1 cha kulia chakula.
·         Arki vanilla kijiko 1 cha kulia chakula.
·         Baking powder vijiko 2 vya kulia chakula.
·         Cocoa au unga wa kahawa vijiko 3 vya kulia chakula.
·         Unga wa mdalasini kijiko 1 cha chai.
·         Mayai yakiwa makubwa 10 na yakiwa madogo 12.
·          Baking tray - Tray ya Kuokea.

namna  ya kutayarisha

·         Weka siagi ndani ya bakuli la kuchanganyia  pamoja na sugari  uichanganye  pamoja mpaka vichanganyike  vizuri (unaweza kuisaga  sukari yako ukitaka lakini si lazima).
·         Ikichanganyika vizuri weka mayai uchanganye pamoja pia  ichanganyike  vizuri.
·         Weka arki zote mbili kwa pamoja huku  ukizichanganya
·         Uchanganye unga na baking powder na uanze kuweka kwenye mchanganyiko wa siagi, mayai  na sukari.
·         Hakikisha unaweka unga wako kidogo kidogo na sio wote kwa wakati mmoja.
·         Ukisha changanyika punguza  mchanganyiko huo robo yake kwenye bakuli jengine na utie unga wa Cocoa au kahawa pamoja na mdalasini na uchanganye  vizuri mpaka ubadilike uwe rangi moja.
·         Ipake  siagi  kwenye baking tray na umimine mchanganyiko wa keki  ambayo haina cocoa robo ya unga na utandaze vizuri.
·         Weka mchanganyiko wako wenye cocoa juu yake pia utandaze vizuri.
·         Malizia kwa kuweka mchanganyiko wa keki iliyokuwa haina cocoa kwa juu tandaza vizuri na tayari kwa kuichoma.
·         Kwa wanaotumia jiko la Gesi ni kipimo cha mark 5 na kwa wale wanotumia jiko la umeme ni mark 250 ya spidi ya jiko.
·         Ili iwive vizuri na kuwa na rangi ya kupendeza inachukua muda wa saa 1  kuokwa na tayari kwa kuliwa.

Kidokezo

Unaweza kutumia mashine ya kusagia keki na kama huna  tumia mwiko tu kwa kuchanganyia na itakuwa nzuri tu usikhofu. Pia isubiri keki  ipoe ndio uitowe kwa kuhofia isije ikakatika wakati wa kuitoa kwenye  tray ya kuokea - baking tray.

Maoni 18 :

  1. Nimeipenca post yako. Umeelezea vizuri. Kuna MAPISHI YA KEKI YA MAZIWA unaweza pata maelezo Yale hapo https://www.bongolives.com/2019/04/mapishi-ya-kupika-keki-ya-maziwa.html

    JibuFuta
  2. Unaeleweka vizuri,je kwa kutumia jiko la mkaa

    JibuFuta
  3. Asante kwa hatua nzuri hadi keki kuiva, nitapika na mimi

    JibuFuta
  4. Nashukuru kwa somo nami nakwenda kupika

    JibuFuta
  5. Asante kwa somo nimeelewa vizuri endelea kutupa maarifa

    JibuFuta
  6. Nimependa unaelezea vizuri sana

    JibuFuta
  7. Habari dada mi naomba msaada hapo keki ya kilo moja unatumia trey ya tin ngap?? Kingine nisaidie nikipika keki haipandi kama hizo nakosea wap yan inaumuka kidogo tu nisaidie ndgu

    JibuFuta
  8. Asanteni kwa darasa lenu tunashukuru tunaelewa tutapika

    JibuFuta
  9. Asantee kwa mafunzo yenu mazuri tunajifunza

    JibuFuta
  10. asante kwa maelekezo mazuri ya jinsi ya kupika keki . Swali je hapo kwenye keki ya unga kilo moja unaweka maji au maziwa kiasi gani?

    JibuFuta
  11. Naitaji kufanya biashara ya keki zile ndogondogo ili niweze kutoka nifanyeje?

    JibuFuta
  12. Habari zenu Asante Kwa mafunzo yenu ila Niko na swali je kama unataka kupika keki ya kilo moja tafadhal Naomba vipimo vya vifaa vyote.Asante

    JibuFuta
  13. Endelea kutufundisha mungu ataongeza kipaji juuu yako

    JibuFuta