Alhamisi, 16 Oktoba 2014

UROJO

Mbatata za Urojo

 
 
Vinavyohitajika

Mbatata  ¼ kilo

Bizari ya manjano ¼ kijiko cha chakula

Ndimu 1 kubwa

Embe mbichi moja

Chumvi

Unga wa ngano vijiko vya chakula 4

Namna ya kutayarisha na kupika

Chemsha mbatata na maganda yake

Zikishawiva, ziepue na uziwache zipoe

Teleka sufuria ya maji kwenye jiko lenye moto pamoja na embe mbichi

Koroga unga kwa maji na bizari uwe kama wa kupikia uji

Maji yakianza kupata moto weka unga na upike kama uji

Uwache uchemke na huku ukiukoroga

Kamua ndimu uweke kwenye urojo pamoja na chumvi

Zimenye mbatata na uzikate vipande vidogo vidogo uweke kwenye bakuli na umimine urojo tayari kwa kuliwa.

Kidokezo

Zinapendeza kuliwa kwa mishikaki ya kuku au nyama. Pia bajia ndio mwenziwe pia usikose chips za muhogo na kachori.

Maoni 1 :

  1. Nimefurahi sana na hii ,imenisaidia nimejiajuri kwa mtaji mdogo, japo bado sijakua ila pesa yakula sikosi nakulipa kodi

    JibuFuta